/ Kutayarisha Kichapishi / Kuweka Nakala za Kwanza / Kuweka Nakala Asili kwenye Glasi ya Kichanganuzi

Kuweka Nakala Asili kwenye Glasi ya Kichanganuzi

Muhimu:

Wakati unaweka nakala nyingi za kwanza kama vile vitabu, zuia mwangaza kutoka nje kumulika kwenye glasi ya kichanganuzi moja kwa moja.

  1. Fungua kifuniko cha hati.

  2. Ondoa vumbi au uchafu wowote ulio kwenye glasi ya kichanganuzi.

  3. Weka nakala ya kwanza ikiangalia chini na uitelezeshe hadi kwa alama ya kona.

    Kumbuka:

    Umbali wa mm 1.5 kutoka kwa ukingo wa chini na ukingo wa upande wa kulia wa glasi ya kichanganuzi haujatambazwa.

  4. Funga kifuniko polepole.

    Muhimu:

    Usitumie nguvu mingi zaidi kwenye glasi ya kichanganuzi au jalada la waraka.Vinginevyo, huenda zikaharibika.

  5. Ondoa nakala za kwanza baada ya kutambaza.

    Kumbuka:

    Ukiwacha nakala za kwanza kwenye glasi ya kichanganuzi kwa muda mrefu, zinaweza kukwama kwenye kioo.