Chaguo za Menyu ya Mipangilio ya Karatasi na Chapisho

Ukubwa wa Karatasi:

Teua ukubwa wa karatasi uliyopakia.

Aina ya Karatasi:

Teua aina ya karatasi uliyopakia.

Mkanda wa Karatasi:

Huonyeza kaseti ya karatasi.

Mpangilio wa Mpaka
  • Isiyo na mipaka:

    Huchapisha bila pambizo kwenye kingo. Picha hupanuliwa kidogo ili kuondoa mipaka kwenye kingo za karatasi.

  • Na mipaka:

    Huchapisha na pambizo nyeupe kwenye kingo.

Upanuzi:

Kwa uchapishaji usio na mpaka, taswira inakuzwa kiasi ili kuondoa mipaka kutoka kwa kingo za karatasi. Teua kiwango cha kukuza taswira.

Tosheza Fremu:

Ikiwa mgao uwiano wa data ya picha na ukubwa wa karatasi ni tofauti, picha hupanuliwa au kupunguzwa kiotomatiki ili pande zile fupi zilingane na pande fupi za karatasi. Upande mrefu wa picha hukatwa ikiwa unazidi upande mrefu wa karatasi. Kipengele hiki huenda kisifanye kazi kwa picha za panorama.

Tarehe:

Chagua umbizo linalotumiwa kuchapisha tarehe kwenye picha kwa picha ambazo zinajumuisha tarehe ambayo picha ilipigwa au tarehe picha hizo zilihifadhiwa. Tarehe haichapishwi kwa baadhi ya mipangilio.

Ondoa Mipangilio Yote:

Huweka upya mipangilio ya karatasi na chapisho kwenye chaguo-msingi yake.