/ Mambo Msingi ya Uchapishaji / Usanidiwa Skrini Msingi / Ikoni Zinazonekana kwenye Skrini ya LCD

Ikoni Zinazonekana kwenye Skrini ya LCD

Ikoni zifuatazo zinaonekana kwenye skrini ya LCD kulingana na hali ya printa.

Huonyesha skrini ya Hali ya Ugavi.

Unaweza kuangalia kiwango cha wino na kiwango cha maisha ya huduma ya kikasha cha ukarabati.

Huonyesha hali ya muunganisho wa mtandao.

Teua ikoni ili kuangalia na kubadilisha mipangilio ya sasa. Hii ni njia mkato kwa menyu ifuatayo.

Mipangilio > Mipangilio ya Mtandao > Usanidi wa Wi-Fi

Kichapishi hiki hakijaunganishwa kwa mtandao wa waya (Ethaneti).

Kichapishi hiki kinatafuta SSID, anwani ya IP ya kukiondoa, au kukumbana na tatizo na mtandao wa pasi waya (Wi-Fi).

Kichapishi kimeunganishwa kwa mtandao wa pasi waya (Wi-Fi).

Idadi ya pau inaonyesha nguvu ya wimbi la muunganisho. Unapokuwa na miambaa mingi, ndivyo muunganisho unaimarika.

Kichapishi hakijaunganishwa kwa mtandao wa pasi waya (Wi-Fi) katika modi ya Wi-Fi Direct (AP Rahisi).

Kichapishi kimeunganishwa kwa mtandao wa pasi waya (Wi-Fi) katika modi ya Wi-Fi Direct (AP Rahisi).

Huonyesha iwapo Hali Tulivu imewekwa klwa kichapishi au la. Kipengele kinapowezeshwa, kelele iliyopigwa na operesheni za kichapishi inapunguika, lakini kasi ya kuchapisha inaweza kupungua. Hata hivyo, huenda kelele isipungue kwenye aina ya karatasi iliyoteuliwa na ubora wa chapisho.

Huonyesha kuwa kuna maelezo ya ziada. Teua ikoni ili kuonyesha ujumbe.

Huonyesha tatizo la vipengee. Teua ikoni ili kuangalia jinsi ya kutatua tatizo.