/ Kunakili / Mbinu Mbalimbali za Kunakili / Kunakili katika Miundo Mbalimbali

Kunakili katika Miundo Mbalimbali

Unaweza kunakili rahisi kwa kuteua menyu kwa malengo yako kama vile kunakili pande zote za kadi ya Kitambulisho kwenyeupande mmoja w karatasi ya ukubwa wa A4, au kunakili kurasa mbili zinazoangaliana za kitabu kwenye laha moja la karatasi.

  1. Weka karatasi katika kichapishi.

  2. Teua Chapa mbalimbali kwenye paneli dhibiti.

    Ili kuteua kipengee, sogeza kulenga kwa kipengee kutumia vitufe vya , na kisha bonyeza kitufe cha OK.

  3. Teua Nakala mbalimbali, na kisha uteue menyu ya kunakili.

    • Kadi ya Kitambulisho
      Hutambaza pande zote mbili za kadi ya utambulisho na hunakili upande mmoja wa karatasi yenye ukubwa wa A4.
    • Nakala ya kitabu
      Hunakili kurasa mbili za A4 zinazoangaliana za kitabu nakadhalika kwenye laha moja la karatasi.
    • Nakala Isiyo na mipaka
      Hunakili bila pambizo kwenye kingo.Taswira imekuzwa kidogo ili kuondoa pambizo kutoka kwenye kingo za karatasi.
  4. Weka nakala za kwanza.

    Kwa Nakala ya kitabu, weka ukurasa wa kwanza wa naka asili ukifuata maagizo yaliyoonyeshwa kwenye skrini, na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  5. Weka mipangilio kwenye kichupo cha Nakili.

    Vipengee vinavyopatikana vinatofautiana kulingana na menyu ya kunakili.

  6. Unda mipangilio kwa kila kipengee kwenye kichupo cha Mipangilio Mahiri inavyohitajika.

  7. Teua kichupo cha Nakili, na kisha uweke idadi ya nakala.

  8. Bonyeza kitufe cha .

    Kumbuka:

    Iwapo utateua Hakiki, unaweza kuangalia taswira zilizotambazwa.

  9. Kwa Kadi ya Kitambulisho au Nakala ya kitabu, fuata maagizo ya kwenye skrini ili kuweka nakala asili zilizosalia, na kisha uteue Anza Kutambaza.