/ Huduma ya Mtandao na Maelezo ya Programu / Programu-tumizi ya Kutambaza na Kuhamisha Taswira (Easy Photo Scan)

Programu-tumizi ya Kutambaza na Kuhamisha Taswira (Easy Photo Scan)

Easy Photo Scan ni programu-tumizi inayokuruhusu kutambaza picha na kutuma kwa urahisi taswira iliyotambazwa kwenye kompyuta au huduma ya wingu.Pia unaweza kurekebisha kwa urahisi taswira iliyotambazwa.Angalia msaada wa programu-tumizi kwa maelezo.

Kumbuka:

Ili utumie programu-tumizi hii, kiendeshi cha kitambazaji Epson Scan 2 kinahitaji kusakinishwa.

Kuanzia kwenye Windows
  • Windows 10

    Bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue Programu ya Epson > Utambazaji Rahisi wa Picha.

  • Windows 8.1/Windows 8

    Andika jina la programu-tumizi katika sehemu ya utafutaji, na kisha uteue ikoni inayoonekana.

  • Windows 7/Windows Vista/Windows XP

    Bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue Programu Zote au Programu > Epson Software > Easy Photo Scan.

Kuanzia kwenye Mac OS

Teua Nenda > Programu > Epson Software > Easy Photo Scan.