/ Kunakili / Mbinu Mbalimbali za Kunakili / Kunakili Picha / Chaguo za Menyu ya Karatasi na Mipangilio ya Kuchapisha kwa Picha za Kunakili

Chaguo za Menyu ya Karatasi na Mipangilio ya Kuchapisha kwa Picha za Kunakili

Rejesha rangi

Hurejesha rangi ya picha zenye rangi hafifu.

Ukubwa wa Karatasi

Teua ukubwa wa karatasi uliyopakia.

Aina ya Karatasi

Teua aina ya karatasi uliyopakia.

Mkanda wa Karatasi

Angalia chanzo cha karatasi ambacho unataka kutumia.

Mpangilio wa Mpaka
  • Isiyo na mipaka

    Hunakili bila pambizo kwenye kingo. Taswira imekuzwa kidogo ili kuondoa pambizo kutoka kwenye kingo za karatasi. Teua kiwango cha kubadilisha ukubwa kwenye mpangilio wa Upanuzi.

  • Na mipaka

    Hunakili kwa pambizo kwenye kingo.

Ondoa Mipangilio Yote:

Huweka upya mipangilio ya nakala kwa chaguo-msingi yake.