/ Kutayarisha Kichapishi / Kuingiza Kadi ya Kumbukumbu / Kufikia Kadi ya Kumbukumbi Kutoka kwenye Kompyuta

Kufikia Kadi ya Kumbukumbi Kutoka kwenye Kompyuta

Unaweza kuandika au kusoma data kwenye kifaa cha hifadhi ya nje kama vile kadi ya kumbukumbu ambayo imechomekwa kwenye kichapishi kutoka kwenye kompyuta.

Muhimu:
  • Chomeka kadi ya kumbukumbu baada ya kuondoa ulinzi wa kuandika.

  • Iwapo taswira imehifadhiwa kwenye kadi ya kumbukumbu kutoka kwenye kompyuta, taswira na idadi ya picha hazionyeshiw upya kwenye skrini ya LCD. Ondoa na uchomeke tena kadi ya kumbukumbu.

  • Unaposhiriki kifaa cha nje kilichochomekwa kwenye kichapishi kati ya kompyuta zilizounganishwa kupitia USB na kwenye mtandao, ufikiaji wa kuandika unaruhusiwa tu kwa kompyuta ambazo zimeunganishwa kwa mbinu uliyoteua kwenye kichapishi. Ili kuandika kwenye kifaa cha hifadhi ya nje, ingiza Mipangilio kwenye paneli kidhibiti na uteue Kushiriki Faili na mbinu ya muunganisho.

Windows

Teua kifaa cha hifadhi ya nje kwenye Kompyuta au Kompyuta Yangu. Data kwenye kifaa cha hifadhi ya nje inaonyeshwa.

Kumbuka:

Ikiwa umeunganisha printa kwenye mtandao bila diski ya programu au Web Installer, kuweka nafasi ya kadi ya kumbukumbu au kituo cha USB kama kiendeshi cha mtandao. Fungua Endesha na uingize jina la kichapishi \\XXXXX au anwani ya IP ya kichapishi \\XXX.XXX.XXX.XXX ili Fungua:. Bofya kulia kwenye ikoni ya kifaa iliyoonyeshwa ili upangie mtandao. Kiendeshi cha mtandao hutokea katika Kompyuta au Kompyuta Yangu.

Mac OS

Teua ikoni inayolingana ya kifaa. Data kwenye kifaa cha hifadhi ya nje inaonyeshwa.

Kumbuka:
  • Ili uondoe kifaa cha hifadhi ya ndani, kokota au dondosha ikoni ya kifaa kwenye ikoni ya takataka. Kama sivyo, huenda data kwenye kiendeshi kilichoshirikiwa kisionyeshwe vizuri wakati kifaa kingine cha hifadhi cha nje kimeingizwa.

  • Ili ufikie kifaa cha hifadhi cha nje kupitia mtandao, chagua Go > Connect to Server kutoka kwa menyu kwenye eneo kazi. Ingiza jina la kichapishi cifs://XXXXX au smb://XXXXX (Ambapo “XXXXX” ni jina la kichapishi) katika Anwani ya Seva, na kisha ubofye Unganisha.