/ Kutayarisha Kichapishi / Kupakia Karatasi / Kupakia Bahasha na Tahadhari

Kupakia Bahasha na Tahadhari

Pakia bahasha wakati upande wa kuchapisha unaangalia juu, na kisha telezesha miongozo ya ukingo wa mbele katika ukingo wa bahasha.

  • Pepeza na upange kingo za bahasha kabla ya kuzipakia. Wakati bahasha zilizokusanywa zimefurishwa na hewa, zifinye chini ili uzifanye tambarare kabla ya kuzipakia.

  • Usitumie bahasha ambazo zimekunjika au kukunjwa. Utumiaji wa bahasha hizi husababisha ukwamaji wa karatasi na uchafu kwenye uchapishaji.

  • Usitumie bahasha zilizo na sura zenye kunata kwenye kifuniko au dirisha la bahasha.

  • Epuka kutumia bahasha ambazo ni nyembamba sana, kwani zinaweza kukunjika wakati wa uchapishaji.