/ Mipangilio ya Mtandao / Aina za Muunganisho wa Mtandao / Muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi)

Muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi)

Tumia mbinu hii ya muunganisho wakati hutumii Wi-Fi nyumbani au afisini, au wakati unataka kuunganisha kichapishi na kompyuta au kifaa maizi moja kwa moja. Katika modi hii, kichapishi hutumika kama eneo la ufikiaji na unaweza kuunganisha hadi vifaa vinne kwenye kichapishi bila kutumia eneo wastani la ufikiaji. Hata hivyo, vifaa vilivyounganishwa moja kwa moja kwenye kichapishi haviwezi kuwasiliana na vingine kupitia kichapishi.

Kumbuka:

Muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi) ni mbinu ya muunganisho iliyobuniwa ili kubadilisha modi ya Kidharura.

Kichapishi kinaweza kuunganishwa na Wi-Fi na muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi) kwa wakati mmoja. Hata hivyo, ukiwasha muunganisho wa mtandao kwenye muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi) wakati kichapishi kimeunganishwa kwa Wi-Fi, Wi-Fi inakatwa muunganisho kwa muda.