/ Kutayarisha Kichapishi / Kuingiza Kadi ya Kumbukumbu / Kuchomeka na Kuondoa Kadi ya Kumbukumbu

Kuchomeka na Kuondoa Kadi ya Kumbukumbu

  1. Chomeka kadi ya kumbukumbu kwenye kichapishi.

    Kichapishi huanza kusoma data na mwangaza unawaka.Wakati usomaji umekamilika, mwangaza husitisha kutoa nuru na kuendelea kuwaka.

    Muhimu:

    Chomeka kadi ya kumbukumbu moja kwa moja kwenye kichapishi.

  2. Unapokamilisha kutumia kadi ya kumbukumbu, hakikisha mwangaza hauwaki, na kisha usukume kadi ili kuiondoa.

    Muhimu:

    Iwapo utaondoa kadi ya kumbukumbu wakati mwangaza unawaka, huenda data kwenye kadi ya kumbukumbu ikapotea.

    Kumbuka:

    Ukifikia kadi ya kumbukumbu kutoka kwenye kompyuta, unahitaji kutumia kompyuta ili uondoe kwa usalama kifaa kinachoweza kuondolewa.