/ Kukarabati Kichapishi / Kulinganisha Kichwa cha Kuchapisha / Kupangilia Kichwa cha Kuchapisha — Paneli Dhibiti

Kupangilia Kichwa cha Kuchapisha — Paneli Dhibiti

  1. Weka karatasi tupu yenye ukubwa wa A4 katika kichapishi.

  2. Teua Matengenezo kwenye skrini ya nyumbani.

    Ili kuteua kipengee, sogeza kulenga kwa kipengee kutumia vitufe vya , na kisha bonyeza kitufe cha OK.

  3. Teua Ulainishaji Kichwa.

  4. Iwapo mistari wima itaonekana kutopangiliwa vizuri au iwapo machapisho yako hayaonekani vizuri, nenda kwenye hatua ya 5. Iwapo utaona bendi ya mlalo kwa vipindi vya kila mara, nenda kwenye hatua ya 11.

  5. Teua Upangiliaji Msingi, na kisha ufuate maagizo yaliyo kwenye skrini ili kuchanpisha ruwaza iliyopangiliwa.

  6. Fuata maelekezo yaliyo kwenye skrini ili kpangilia kichwa cha kuchapisha.

    Tafuta na uteue idadi ya ruwaza ambayo ina mstari michache wima isiyopangiliwa vizuri.

  7. Teua Ulainishaji Wima, na kisha uchapishe ruwaza iliyopangiliwa.

  8. Tafuta na uteue nambari ya ruwaza imara zaidi katika kila kikundi.

  9. Teua Mpangilio uliopigwa Mstari, na kisha uchapishe ruwaza iliyopangiliwa.

  10. Tafuta na uteue idadi ya ruwaza ambayo ina mstari michache wima isiyopangiliwa vizuri.

    Upangiliaji umekamilika.

  11. Teua Upangiliaji Kimlalo, na kisha ufuate maagizo yaliyo kwenye skrini ili kuchanpisha ruwaza iliyopangiliwa.

  12. Fuata maelekezo yaliyo kwenye skrini ili kpangilia kichwa cha kuchapisha.

    Tafuta na uteue nambari ya ruwaza iliyogawanywa na inayopishana.