Chaguo za Menyu za Kuhariri Picha

(Pogoa):

Hupogoa sehemu ya picha. Unaweza kusogeza, kukuza, au kupunguza eneo la kupogoa.

(Kichujio):

Uchapishaji katika sepia au monokromu.

(Marekebisho):

Hutekeleza suluhisho za rangi kutumia Boresha au kipengele cha Ta. Jicho Ny'u.

Boresha:

Teua mojawapo ya chaguo za kurekebisha picha. Otomatiki, Watu, Mandhari, au Mandhari Usiku hutoa picha nzuri zaidi na rangi dhahiri zaidi kwa kurekebisha ulinganuaji, ukifishwaji, na uangavu wa data ya kwanza ya picha kiotomatiki.

  • Otomatiki:

    Kichapishi hutambua maudhui ya taswira na kuboresha taswira kiotomatiki kulingana na maudhui yaliyotambuliwa.

  • Watu:

    Inapendekezwa kwa taswira za watu.

  • Mandhari:

    Imependekezwa kwa taswira au mandhari.

  • Mandhari Usiku:

    Imependekezwa kwa taswira au mandhari ya usiku.

  • Ub'aji Umezimwa:

    Huzima kipengele cha Boresha.

Ta. Jicho Ny'u:

Hurekebisha jicho jekundu kwenye picha. Marekebisho hayatekelezwi kwenye faili asili, kwenye machapisho tu. Kulingana na aina ya picha, sehemu za picha kando na macho zinaweza kurekebishwa.

Ung’avu:

Rekebisha ung’avu wa taswira.

Ulinganuzi:

Hurekebisha tofauti kati ya mwangaza na giza.

Ukali:

Huboresha au kuondoa ulengaji wa muhtasari wa taswira.

Kulowesha:

Rekebisha uwazi wa taswira.