/ Kunakili / Mbinu Mbalimbali za Kunakili / Kunakili Picha

Kunakili Picha

Unaweza kunakili picha nyingi kwa ukuzaji mmoja.Pia unaweza kurejesha rangi katika picha zilizofifia.

Ukubwa wa chini zaidi wa nakala asili unaweza kunakini ni 30×40 mm.

Kumbuka:

Huenda nafasi nyeupe iliyo karibu na picha isitambuliwe.

  1. Weka karatasi katika kichapishi.

  2. Teua Chapa mbalimbali kwenye skrini ya nyumbani.

    Ili kuteua kipengee, sogeza kulenga kwa kipengee kutumia vitufe vya , na kisha bonyeza kitufe cha OK.

  3. Teua Nakala mbalimbali > Nakili/Rejesha Picha.

  4. Badilisha mipangilio ya chapisho inavyohitajika, na kisha ubonyeze kitufe cha .

  5. Weka picha kwenye glasi ya kichanganuzi, na kisha uteue Anza Kutambaza.

    Picha zinatambazwa na kuonyeshwa kwenye skrini.

  6. Bonyeza iwapo inahitajika kuunda mipangilio kama vile marekebisho ya picha.

    Kumbuka:

    Iwapo unataka kuchapisha kwa kuongeza ukubwa wa sehemu ya picha, teua Puna/Kuza, na kisha uunde mipangilio.Telezesha eneo la kuchapisha ukitumia vitufe vya , na kisha ubadilishe ukubwa wa fremu kwa kutumia kitufe cha + au -.

  7. Ingiza idadi ya nakala iwezekanavyo, na kisha ubonyeze kitufe cha .