/ Kuchapisha / Kuchapisha Kutoka kwa Vifaa Mahiri / Kutumia Epson iPrint / Kuchapisha Picha Ukitumia Epson iPrint

Kuchapisha Picha Ukitumia Epson iPrint

Anzisha Epson iPrint kutoka kwa kifaa chako mahiri na uchague kipengele unachotaka kutumia kutoka kwa skrini ya nyumbani.

Skrini zifuatazo zinaweza kubadilishwa bila ilani. Maudhui yanaweza kutofautiana kulingana na bidhaa.

Skrini ya nyumbani inayoonekana wakati programu-tumizi imeanzishwa.

Huonyesha maelezo kuhusu jinsi ya kusanidi kichapishi na Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara.

Huonyesha skrini unapoweza kuteua kichapishi na kuweka mipangilio ya kichapishi. Ukishateua kichapishi, huhitaji kuichagua ten wakati ujao.

Teua unachotaka kuchapisha kama vile picha na nyaraka.

Skrini ya kuchapisha picha inayoonyeshwa wakati menyu ya picha imeteuliwa.

Huonyesha skrini ya kuweka mipangilio ya uchapishaji kama vile ukubwa wa karatasi na aina ya karatasi.

Huonyeza ukubwa wa karatasi. Wakati hii imeonyeshwa kama kitufe, kidonoer ili uonyeshe mipangilio ya karatasi iliyowekwa kwa sasa kwenye kichapishi.

Huonyesha picha na hati ulizoteua.

Huanzisha uchapishaji.

Kumbuka:

Ili uchapishe kutoka kwa menyu ya hati iPhone, iPad, na iPod touch inayotumia iOS, anzisha Epson iPrint ukitumia baada ya kuhamisha hati unayotaka kuchapisha ukitumia dhima ya kushiriki faili katika iTunes.