Menyu zinazopatikana hutofautiana kulingana na mpangilio unaochagua.
Ingiza idadi ya nakala.
Hunakili nakala asili katika rangi.
Hunakili nakala asili katika rangi nyeusi na nyeupe (rangi moja).
1>Upande 1
Hunakili upande mmoja wa hati halisi kwenye karatasi ya upande moja.
1>Pande 2
Hunakili hati halisi zenye pande mbele kwenye pande mbili za karatasi moja. Teua mwelekeo wa nakala asili na eneo la kuunganisha karatasi.
Ongeza kiwango cha uzito wakati matokeo ya kunakili yamefifia. Punguza kiwango cha uzito wino unapomwagika.
Weka ukubwa na aina ya karatasi uliyoweka Kuchapisha katika kichapishi.
Hukuza au kupunguza nakala asili.
Ukubwa Halisi
Hunakili kwa ukuzaji wa 100%.
Tosheza Kiotomati
Hutambua eneo la kuchapisha na kukuza kiotomatiki au kupunguza nakala asili ili itoshee kwenye ukubwa wa karatasi uliyoteua. Wakati kuna pambizo nyeupe kwenye nakala asili, pambizo hizo nyeupe kutoka kwenye alama ya kona ya glasi ya kichanganuzi zinatambuliwa kama eneo la kutambaza, lakini pambizo katika upande mkabala zinaweza kupunwa.

Maalum
Teua ili kubainisha ukuzaji ili kuongeza au kupunguza nakala asili.
Hubainisha ukuzaji unaotumika kuongeza au kupunguza nakala asili ndani ya masafa ya 25 hadi 400%.
Chagua ukubwa wa nakala yako ya kwanza. Unaponakili nakala asili za ukubwa usio wastani, teua ukubwa unaokaribiana na nakala yako asili.
Ukurasa Mmoja
Hunakili hati halisi zenye pande mbili kwenye karatasi moja.
2-juu
Hunakili hati halisi zenye pande mbili kwenye karatasi moja yenye mpangilio wa 2-up. Teua mpangilio wa muundo na mwelekeo wa nakala yako asili.
Teua ubora wa kuchapisha. Rasimu hutoa uchapishaji wa haraka zaidi, lakini uchapishaji huenda ukawa fifu. Bora hutoa uchapishaji wa hali ya juu zaidi, lakini kasi ya uchapishaji huenda ikawa polepole.
Kwa watumiaji wa Ulaya Magharibi, modi ya mswadajaribio haipatikani.
Hutambaza pande zote mbili za kadi ya utambulisho na hunakili upande mmoja wa karatasi yenye ukubwa wa A4.
Hunakili bila pambizo kwenye kingo. Taswira imekuzwa kidogo ili kuondoa pambizo kutoka kwenye kingo za karatasi. Teua kiwango cha kubadilisha ukubwa kwenye mpangilio wa Upanuzi.
Kwa uchapishaji usio na mpaka, taswira inakuzwa kiasi ili kuondoa mipaka kutoka kwa kingo za karatasi. Teua kiwango cha kukuza taswira.