/ Mipangilio ya Mtandao / Kuunda Mipangilio ya Wi-Fi kwenye Kichapishi / Kuunda Mipangilio ya Wi-Fi kwa Usanidi wa Kitufe cha Kusukuma

Kuunda Mipangilio ya Wi-Fi kwa Usanidi wa Kitufe cha Kusukuma

Unaweza kusanidi kiotomatiki mtandao wa Wi-Fi kwa kubonyeza kitufe kwenye kipanga njia pasiwaya. Ikiwa masharti yafuatayo yatatimizwa, unaweza kusanidi kwa kutumia mbinu hii.

  • Kipamnga njia pasiwaya kinatangamana na WPS (Usanidi wa Wi-Fi Uliolindwa).

  • Muunganisho wa sasa wa Wi-Fi ulitambuliwa kwa kubonyeza kitufe kwenye kipanmga njia pasiwaya.

  1. Teua Usanidi wa Wi-Fi kwenye skrini ya nyumbani.

    Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya , na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  2. Teua Wi-Fi (Inapendekezwa).

  3. Bonyeza kitufe cha OK ili kuendelea.

  4. Teua Sukuma Kitufe cha Usanidi (WPS).

  5. Shikilia chini kitufe cha [WPS] kwenye kipanga njia pasiwaya hadi taa ya usalama imweke.

    Ikiwa hujui kilipo kitufe cha [WPS], au hakuna vitufe kwenye kipanga njia pasiwaya, tazama hati iliyotolewa yenye eneo la ufikiaji kwa maelezo.

  6. Bonyeza kitufe cha OK kwenye paneli dhibiti ya kichapishi. Fuata maagizo yaliyo kwenye skrini yaliyo hapa.

    Kumbuka:

    Iwapo muunganisho utashindikana, washa upya kipanga niia pasiwaya, kisogeze karibu na kichapishi, na ujaribu tena. Iwapo haitafanya kazi, chapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao na uangalie suluhisho.