/ Kutatua Matatizo / Matatizo ya Picha Iliyotambazwa / Matini Hayatambuliwi Sahihi Unapohifadhi kama PDF Zinazoweza kutafutwa

Matini Hayatambuliwi Sahihi Unapohifadhi kama PDF Zinazoweza kutafutwa

  • Kwenye dirisha la Chaguo la Fomati ya Picha katika Epson Scan 2, hakikisha kuwa Lugha ya Maandishi imewekwa sahihi kwenye kichupo cha Maandishi.

  • Hakikisha kuwa nakala asili imewekwa wima.

  • Tumia nakala asili iliyo na matini yanayoonekana vizuri. Huenda utambuzi wa matini ukakataa kwa aina zifuatazo za nakala asili.

    • Nakala asili zilizonakiliwa mara nyingi

    • Nakala asili zilizopokewa kwa faksi (katika ulinganuzi wa chini)

    • Nakala asili ambapo uwekaji nafasi ya herufi au mstari ni ndogo zaidi

    • Nakala asili zizlizo na mistari au mistari ya chini juu ya matini

    • Nakala asili zilizo na matini yaliyoandikwa kwa mkono

    • Nakala asili zilizo na mikunjo au kasoro

  • Kwenye Hali ya Hati katika Epson Scan 2, wakati Aina ya Picha kwenye kichupo cha Mipangilio Kuu imewekwa kwa Ny'i na Nyeupe, rekebisha Kiwango cha juu kwenye kichupo cha Mipangilio ya hali ya Juu. Unapoongeza Kiwango cha juu, rangi nyeusi huwa thabiti.

  • Kwenye Hali ya Hati katika Epson Scan 2, teua kichupo cha Mipangilio ya hali ya Juu, na kisha Chaguo la Picha > Uboreshaji Maandishi.