Mipan. Kutuma Faksi

Teua menyu kwenye paneli dhibiti kama ilivyofafanuliwa hapa chini:

Faksi > Menyu > Mipan. Kutuma Faksi

Tuma Moja kwa Moja

Hutuma faksi ya rangi moja inapotambaza nakala asili. Kwa kuwa nakala asili zilizotambazwa hazihifadhiwi kwa muda kwenye kumbukumb u ya kichapishi hata wakati wa kutuma kiwango kikubwa cha kurasa, unaweza kuzuia makosa ya kichapishi kwa sababu ya kutokuwa na kumbukumbu. Kumbuka kuwa kutuma kwa kutumia kipengele hiki huchukua muda mrefu kuliko kutotumia kipengele hiki. Tazama “Maelezo Husiani” hapa chini kuhusu mada hii.

Huwezi kutumia kipengele hiki wakati unatuma faksi kwa wapokeaji wengi.

Tuma Faksi Baadaye

Hutuma faksi wakati ambao ulibainisha. Faksi ya rangi moja tu ndio inayopatikana wakati unatumia chaguo hili. Tazama “Maelezo Husiani” hapa chini kuhusu mada hii.

Ongeza Ma. Mtu'ji

Teua eneo ambalo unataka kujumuisha maelezo ya kijajuu (jina la mtumaji na nambari ya faksi) kwenye faksi inayoondoka, au kutojumuisha maelezo.

  • Zima: Hutuma faksi isiyokuwa na maelezo ya kijajuu.

  • Nje ya Picha: Hutuma faksi pamoja na maelezo ya kijajuu katika pambizo nyeupe ya juu ya faksi. Hii huzuia kijajuu kupitana na taswira iliyotambazwa, hata hivyo, faksi iliyopokewa na mpokeaji inaweza kuchapishwa katika laha mbili kulingana na ukubwa wa nakala asili.

  • Ndani ya Picha: Hutuma faksi kwa maelezo ya kijajuu karibu 7 mm chini kuliko upande wa juu wa taswira iliyotambazwa. Kijajuu kinaweza kupitana na taswira, hata hivyo, faksi iliyopokewa na mpokeaji haitagawanywa kwa nyaraka mbili.

Kijajuu cha Faksi

Teua kijajuu kwa mpokeaji. Ili kutumia kipengele hiki, lazima usajili vijajuu anuwai mapema.

Mael. Ziada ya Kijajuu

Teua maelezo unayotaka kuongeza. Unaweza kuteua moja kutoka kwa Nambari Yako ya Simu na Orodha ya Mfikio.

Ripoti ya Upitishaji

Huchapisha ripoti ya usambazaji baada ya wewe kutuma faksi.

Kosa la Chapisho huchapisha ripoti wakati kosa hutokea tu.