Mipangilio ya Uchapishaji

Kwenye kichupo cha kiendishi cha kichapishi cha Chaguo Zaidi, teua Kaida kama mpangilio wa Usahihishaji wa Rangi. Bofya Iliyoboreshwa ili kufungua dirisha la Usahihishaji wa Rangi, na kisha uteue mbinu ya usahihishaji wa rangi.

Kumbuka:
  • Otomatiki inateuliwa kama chaguo-msingi kwenye kichupo cha Chaguo Zaidi. Ukiwa na mpangilio huu, rangi zitarekebishwa kiotomatiki ili zilingane na aina ya karatasi na mipangilio ya ubora wa uchapishaji.

  • Ubora Picha kwenye dirisha la Usahihishaji wa Rangi hurekebisha rangi kwa kuchanganua eneo la kipengele. Kwa hivyo, ikiwa umebadilisha eneo la kipengele kwa kupunguza, kukuza, kupogoa, au kuzungusha picha hiyo, rangi inaweza kubadilika bila kutarajiwa. Uchaguaji wa mpangilio wa bila-kingo pia hubadilisha eneo la kipengele na husababisha mabadiliko ya rangi. Ikiwa picha iko nje ya mwimo, toni inaweza kuwa sio ya kiasili. Ikiwa rangi imebadilishwa au imekuwa sio ya asili, chapisha kwa modi nyingine mbali na Ubora Picha.