Kichupo cha Kuu

Uwekaji Kabla Uchapishaji

Uwekaji upya wa Kuongeza/Kuondoa

Unaweza kuongeza au kuondoa uwekaji awali wako kwa mipangilio ya kuchapisha inayotumika kila mara. Teua uwekaji awali unaotaka kutumia kutoka kwenye orodha.

Onyesha Mipangilio

Huonyesha orodha ya vipengee vilivyowekwa sasa kwenye vichupo vya Kuu na Chaguo Zaidi.

Weka upya Chaguo-msingi

Rudisha mipangilio yote kwenye thamani zake chaguo-msingi ya kiwanda. Mpangilio kwenye kichupo cha Chaguo Zaidi pia inawekwa katika chaguo-msingi yake.

Viwango vya Wino

Huonyesha makadirio ya viwango vya wino.

Chanzo cha K'tasi

Teua chanzo cha karatasi ambacho karatasi huingizwa. Teua Uteuzi Otomatiki ili kuteua kiotomatiki chanzo cha karatasi kilichoteuliwa kwenye mipangilio ya kuchapisha kwenye paneli dhibiti ya kichapishi.

Iwapo kichapishi kina chanzo kimoja tu cha karatasi, kipengee hiki hakionyeshwi.

Ukubwa wa Waraka

Teua ukubwa wa karatasi unayotaka kuchapishwa. Iwapo utateua Mtumiaji-Amefafanuliwa, ingiza upana na urefu wa karatasi.

Isiyo na kingo

Hukuzwa kiasi kidogo zaidi ya ukubwa wa karatasi ili kusiwe na pambizo zinachapishwa kando ya kingo za karatasi. Bofya Mipangilio ili uteue kiwango cha ukuzaji.

Mwelekeo

Teua mwelekeo unaotaka kutumia ili kuchapisha.

Aina ya Krtasi

Teua aina ya karatasi unayochapisha.

Ubora

Teua ubora wa chapisho unaotaka kutumia kwa uchapishaji. Mipangilio inayopatikana inalinganana aina ya karatasi unayoteua. Bofya Mipangilio Zaidi ili uunde mipangilio zaidi.

Rangi

Teua rangi ya kazi yako ya kuchapisha.

Uchapishaji wa Pande 2

Hukuruhusu kutekeleza uchapishaji wa pande 2.

Settings

Unaweza kubainisha ukingo wa kuunganisha na pambizo za kuunganisha. Unapochapisha nyaraka za kurasa nyingi, unaweza kuteua kuchapisha kuanzia upande wa mbele au upande wa nyuma wa ukurasa.

Uzito wa Uchapishaji

Teua aina ya waraka ili kurekebisha uzito wa chapisho. Iwapo uzito wa chapisho unaofaa umeteuliwa, unaweza kuzuia picha kutokea upande wa nyuma. Teua User Defined ili kurekebisha uzito wa chapisho kikuli.

Kurasa Nyingi

Hukuruhusu kuchapisha kurasa nyingi kwenye laha moja au kutekeleza uchapishaji wa bango. Bofya Mpangilio Kurasa ili kubainisha utaratibu ambao kurasa zinachapishwa.

Copies

Weka idadi ya nakala unazotaka kuchapisha.

Pangiliza

Huchapisha nyaraka nyingi zilizolinganishwa kwa utaratibu na kupangwa kwenye vikundi.

Mpangilio Kinyume

Hukuruhusu kuchapisha kutoka ukurasa wa mwisho ili kurasa zikusanywe kulingana na mpangilio sahihi baada ya kuchapisha.

Modi Tulivu

Hupunguza kelele ambayo kicvhapishi hutoa. Hata hivyo, uwezeshaji wa hii unaweza kupunguza kasi ya uchapishaji.

Uhakiki wa Chapisho

Huonyesha uhakiki wa waraka wako kabla ya kuchapisha.

Laiti ya Kipangaji cha Kazi

Teua chapisho kwa kutumia kipengele cha Laiti ya Kipangaji cha Kazi.