Haiwezi Kupokea Faksi

  • Ikiwa umejisajili kwa huduma ya kusambaza simu, huenda printa isiweze kupokea faksi. Wasiliana na mtoa huduma.

  • Ikiwa hujaunganisha simu kwenye printa, weka mpangilio wa Hali ya Kupokea uwe Otomatiki kwenye paneli dhibiti.

  • Chini ya hali zifuatazo, printa huishiwa na kumbukumbu na haiwezi kupokea faksi. Angalia utatuaji kwa maelezo kuhusu kushughulikia hitilafu ya kumbukumbu kujaa.

    • Idadi ya nyaraka zilizopokewa imefika kiwango cha juu cha nyaraka 100.

    • Kumbukumbu ya printa imejaa (100%).

  • Hakikisha iwapo nambari ya faksi ya mtumaji imesajiliwa kwenye Or. N'ari Zil'kataliwa. Faksi zilizotumwa kutoka kwenye nambari ambazo zimeongezwa kwenye orodha hii zimezuiwa wakati Or. N'ari Zil'kataliwa kwenye Faksi ya Kukataliwa imewezeshwa.

  • Uliza mtumaji iwapo maelezo ya kijajuu yamesanidiwa kwenye mashine yake ya faksi. Faksi ambazo hazijumuishi maelezo ya kijajuu yamezuiwa wakati Kij. Faksi kiko Tupu kwenye Faksi ya Kukataliwa imewezeshwa.

  • Angalia iwapo nambari ya faksi ya mtumaji imesajiliwa kwenye orodha ya mwasiliani. Faksi zilizotumwa kutoka kwenye nambari ambazo hazijasajiliwa kwenye orodha hii zimezuiwa wakati Mp. simu hay. ktk W'ni kwenye Faksi ya Kukataliwa imewezeshwa.