/ Kuchapisha / Kuchapisha Kutoka kwa Vifaa Mahiri / Kutumia Epson Print Enabler

Kutumia Epson Print Enabler

Unaweza kuchapisha nyaraka, barua pepe, picha, na kurasa zako za wavuti pasi waya kutoka kwenye simu au kompyuta yako ndogo ya Android (Android v4.4 au jipya zaidi). Kwa haatua chache, kifaa chako cha Android kitatatmbua kichapishi cha Epson ambacho kimeunganishwa kwa mtandao sawa wa pasi waya.

Kumbuka:

Uendeshaji unaweza kutofautiana kulingana na kifaa.

  1. Weka karatasi katika kichapishi.

  2. Sanidi kichapishi chako kwa uchapishi wa pasi waya.

  3. Kwenye kifaa chako cha Android, sakinisha programu-jalizi ya Epson Print Enabler kutoka kwa Google Play.

  4. Unganisha kifaa chako cha Android kwenye mtandao sawa wa pasi waya kama wa kichapishi chako.

  5. Nenda kwenye Mipangilio kwenye kifaa chako cha Android, teua Vifaa vilivyounganishwa > Kuchapisha, na kisha uwezeshe Epson Print Enabler.

  6. Kutoka kwa programu-tumizi ya Android kama vile Chrome, donoa ikoni ya menyu na uchapishe chochote kilicho kwenye skrini.

    Kumbuka:

    Iwapo hutaona kichapishi chako, donoa Vichapishi Vyote na uteue kichapishi chako.