Mambo Msingi ya Uchapishaji

Kumbuka:

Utendaji unaweza kutofautiana kulingana na programu. Angalia msaada wa programu kwa maelezo.

  1. Fungua faili unayotaka kuchapisha.

    Pakia karatasi katika kichapishi iwapo bado haijapakiwa.

  2. Teua Chapisha au Usanidi wa Uchapishaji katika menyu ya Faili.

  3. Teua kichapishi chako.

  4. Teua Mapendeleo au Sifa ili uende kwa dirisha la kiendeshi cha printa.

  5. Badilisha mipangilio kama inavyohitajika.

    Tazama chaguo za menyu kwa kiendeshi cha kichapishi kwa maelezo.

    Kumbuka:
    • Pia unaweza kuona msaada wa mtandaoni kwa ufafanuzi wa vipengele vya mpangilio. Kubofya kulia kipengee huonyesha Msaada.

    • Unapoteua Uhakiki wa Chapisho, unaweza kuona uhakiki wa waraka wako kabla ya kuchapisha.

  6. Bofya Sawa ili ufunge dirisha la kiendeshi cha kichapishi.

  7. Bofya Chapisha.

    Kumbuka:

    Unapoteua Uhakiki wa Chapisho, darisha la uhakiki linaonyeshwa. Ili kubadilisha mipangilio, bofya Ghairi, na kisha urudie utaratibu kutoka hatua ya 2.