/ Mipangilio ya Mtandao / Kuangalia Hali ya Muunganisho ya Mtandao / Kuchapisha Ripoti ya Muunganisho wa Mtandao

Kuchapisha Ripoti ya Muunganisho wa Mtandao

Unaweza kuchapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao ili kuangalia hali kati ya kichapishi na kipanga njia pasiwaya.

  1. Pakia karatasi.

  2. Teua Mipangilio kutoka kwa skrini ya mwanzo, na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

    Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya , na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  3. Teua Mipangilio ya Mtandao > Ukaguzi wa Muunganisho.

    Ukaguzi wa muunganisho unaanza.

  4. Bonyeza kitufe cha ili kuchapisha ripoti ya muunganisho wa mtandao.

    Iwapo kosa limetokea, angalia ripoti ya muunganisho, na kisha ufuate suluhisho zilizochapishwa.