/ Kutatua Matatizo / Haiwezi Kuanzisha Utambazaji

Haiwezi Kuanzisha Utambazaji

  • Unganisha kebo ya USB vizuri kwenye kichapishi na kompyuta. Ikiwa unatumia kitovu cha USB, jaribu kuunganisha kichapishi moja kwa moja kwenye kompyuta.

  • Ukitambaza katika mwonekano wa hali ya juu kwenye mtandao, huenda kosa la mawasiliano likatokea. Punguza mwonekano.

  • Hakikisha kuwa kichapishi (kitambazaji) sahihi kimeteuliwa kwenye Epson Scan 2.

Angalia iwapo kichapishi kimetambuliwa unapotumia Windows au la

Katika Windows, hakikisha kichapishi (kitambazaji) kinaonekana katika Kitambazaji na Kamera. Kichapishi (kitambazaji) kinafaa kionekane kama “EPSON XXXXX (jina la kichapishi)”. Ikiwa kichapishi (kitambazaji) hakionekani, sakinusha Epson Scan 2 na kisha uisakinishe upya. Angalia yafuatayo ili ufikie Kitambazaji na Kamera.

  • Windows 10

    Bofya kitufe cha kuwasha na uteue Mfumo wa Windows > Paneli Dhibiti, ingiza “Kitambazaji na Kamera” katika sehemu ya utafutaji, bofya Tazama vitambazaji na kamera, na kisha uangalie kama kichapishi kinaonekana.

  • Windows 8.1/Windows 8/Windows Server 2012 R2/Windows Server 2012

    Teua Eneo kazi > Mipangilio > Paneli Dhibiti, ingiza “Kitambazaji na Kamera” katika sehemu ya utafutaji, bofya Onyesha Kitambazaji na Kamera, na kisha uangalie kama kichapishi kinaonekana.

  • Windows 7/Windows Server 2008 R2

    Bofya kitufe cha kuwasha na uteue Paneli Dhibiti, ingiza “Kitambazaji na Kamera” katika sehemu ya utafutaji, bofya Tazama vitambazaji na kamera, na kisha uangalie kama kichapishi kinaonekana.

  • Windows Vista/Windows Server 2008

    Bofya kitufe cha kuanza, teua Paneli Dhibiti > Maunzi na Sauti > Vitambazaji na Kamera, na kisha uangalie kama kichapishi kinaonekana.

  • Windows XP/Windows Server 2003 R2/Windows Server 2003

    Bofya kitufe cha kuwasha, teua Paneli Dhibiti > Vichapishi na Maunzi Nyingine > Kitambazaji na Kamera, na kisha uangalie kama kichapishi kinaonekana.