/ Huduma ya Mtandao na Maelezo ya Programu / Programu-tumizi ya Kutuma Faksi (Kiendeshi chaPC-FAX)

Programu-tumizi ya Kutuma Faksi (Kiendeshi chaPC-FAX)

Kiendeshi cha PC-FAX ni programu inakuwezesha kutuma hati iliyoundwa kwenye programu tofauti kama faksi moja kwa moja kutoka kwa kompyuta. Kiendeshi cha PC-FAX husakinishwa wakati unasakinisha Huduma ya FAKSI. Angalia msaada wa programu kwa maelezo.

Kumbuka:
  • Programu endeshi za Windows Server hazikubaliwi.

  • Utendaji huwa tofauti kulingana na programu uliyotumia kuunda hati hiyo. Angalia msaada wa programu kwa maelezo.

Kufikia kutoka kwa Windows

Katika programu, chagua Chapisha au Usanidi wa Uchapishaji katika menyu ya Faili. Chagua printa yako (FAKSI), na kisha ubofye Mapendeleo au Sifa.

Kufikia kutoka kwa Mac OS

Katika programu, chagua Chapisha kutoka kwa menyu ya Faili. Chagua printa yako (FAKSI) kama mpangilio wa Printa, na kisha uchague Fax Settings au Recipient Settings katika menyu ya kidukizo.