/ Kutatua Matatizo / Kuondoa Karatasi Iliyokwama / Kuondoa Karatasi Iliyokwama Kutoka Ndani ya Kichapishi

Kuondoa Karatasi Iliyokwama Kutoka Ndani ya Kichapishi

Tahadhari:
  • Chunga mkono au vidole vyako visikwame wakati unafungua au kufunga kitengo cha kitambazaji. La sivyo unaweza kujeruhiwa.

  • Usiwahi kugusa vitufe vilivyo kwenye paneli dhibiti wakati mkono wako uko ndani ya kichapishi. Ikiwa kichapishi kitaanza kufanya kazi, inaweza kusababisha majeraha. Kuwa makini usiguse sehemu zinazojitokeza ili uzuie majeraha.

  1. Fungua kitengo cha kitambazaji wakati jalada la waraka limefungwa.

  2. Ondoa karatasi iliyokwama.

    Muhimu:

    Usiguse kebo tambarare nyeupe au sehemu angavu iliyo ndani ya kichapishi. Ukifanya hivyo unaweza kusababisha hitalifu.

  3. Funga kitengo cha kitambazaji.

    Kwa usalama, kitengo cha kitambazaji kinafungwa kwa hatua mbili.

    Kumbuka:

    Kitengo cha kitambazaji hakiwezi kufunguliwa kutoka katika nafasi iliyoonyeshwa hapa chini. Kifunge kabisa kabla ya kukifungua.