/ Utambazaji / Utambazaji Kupitia Paneli Dhibiti / Utambazaji kwa Kompyuta / Kuunda Mipangilio Maalum kwenye Epson Event Manager

Kuunda Mipangilio Maalum kwenye Epson Event Manager

Unaweza kuweka mipangilio ya kutambaza ya Kwenye Kompyuta (Maalum) kwenye Epson Event Manager.

Angalia msaada wa Epson Event Manager upate maelezo.

  1. Anzisha Epson Event Manager.

  2. Hakikisha kuwa kitambazaji chako kimeteuliwa kama Scanner kwenye kichupo cha Button Settings katika skrini kuu.

  3. Bofya Make Job Settings.

  4. Weka mipangilio kutambaza kwenye skrini ya Job Settings.

    • Edit Job Settings: Teua Custom Action.
    • Setting: Tambaza kutumia mipangilio bora kwa aina asili iliyoteuliwa. Bofya Detailed Settings for Scanning ili kuweka vipengee kama vile mwonekano au rangi ya kuhifadhi taswira iliyotambazwa.
    • Target Folder: Teua kabrasha la kuhifadhi taswira iliyotambazwa.
    • Filename (Prefix + Start Number): Badilisha mipangilio ya jina la faili unayotaka kuhifadhi.
    • File Format: Teua umbizo la kuhifadhi.
    • Launch Action: Teua hatua wakati wa kutambaza.
    • Test Settings: Anza jaribio la kutambaza kutumia mipangilio ya sasa.
  5. Bofya OK ili kurudi kwenye skrini kuu.

  6. Hakikisha kuwa Custom Action imeteuliwa kwenye orodha ya Custom Action.

  7. Bofya Close ili kufunga Epson Event Manager.