/ Mipangilio ya Mtandao / Kuunganisha kwenye Kifaa Mahiri / Kuunganisha kwenye Vifaa kando na iOS na Android kwa kutumia Wi-Fi Direct

Kuunganisha kwenye Vifaa kando na iOS na Android kwa kutumia Wi-Fi Direct

Mbinu hii hukuruhusu kuunganisha kichapishi moja kwa moja kwenye vifaa maizi bila kipanga njia pasiwaya.

Kumbuka:

Unahitaji kuunda mipangilio hii kwa kichapishi na kifaa maizi unachotaka kuunganisha mara moja. Isipokuwa ulemaze Wi-Fi Direct au kurejesha mipangilio ya mtandao kwa chaguo-msingi yake, huhitaji kuunda mipangilio hii tena.

  1. Teua Usanidi wa Wi-Fi kwenye skrini ya nyumbani.

    Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya , na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  2. Teua Wi-Fi Direct.

  3. Angalia ujumbe, na kisha ubonyeze kitufe cha Sawa ili kuendelea.

  4. Angalia ujumbe, na kisha ubonyeze kitufe cha Sawa ili kuendelea.

  5. Teua Vifaa Vingine vya OS.

    Jina la Mtandao na Nenosiri kwa Wi-Fi Direct vya kichapishi vinaonyeshwa.

  6. Kwenye skrini ya Wi-Fi ya kifaa maizi, teua SSID iliyoonyeshwa kwenye paneli dhibiti, na kisha uingize nenosiri.

    Picha ya skrini ni mfano kwenye iPhone.

  7. Kwenye paneli dhibiti ya kichapishi, bonyeza kitufe cha Sawa.

  8. Kwenye kifaa maizi, washa programu ya uchapishaji ya Epson.

    Mifano ya programu za uchapishaji za Epson

  9. Kwenye skrini ya programu ya uchapishaji ya Epson, donoa Printer is not selected.

  10. Teua kichapishi unachotaka kuunganisha.

    Tazama maelezo yaliyoonyeshwa kwenye paneli dhibiti ya kichapishi ili kuteua kichapishi.

  11. Kwenye paneli dhibiti ya kichapishi, bonyeza kitufe cha Sawa.

Kwa vifaa maizi ambavyo vimeunganishwa kwenye kichapishi mbeleni, teua jina la mtandao (SSID) kwenye skrini ya Wi-Fi ya kifaa maizi ili kuviunganisha tena.