Kuendesha Web Config kwenye Windows

Unapounganisha kompyuta kwenye kichapishi kwa kutumia WSD, fuata hatua hapa chini ili kuendesha Web Config.

  1. Fungua orodha ya vichapishi kwenye kompyuta.

    • Windows 10
      Bofya kitufe cha kuwasha kisha uchague Mifumo ya Windows > Paneli Dhibiti > Tazama vifaa na vichapishi katika Maunzi na Sauti.
    • Windows 8.1/Windows 8
      Teua Eneo-kazi > Mipangilio > Paneli Dhibiti > Tazama vifaa na vichapishi katika Maunzi na Sauti (au Maunzi).
    • Windows 7
      Bofya kitufe cha kuwasha, na uteue Paneli Dhibiti > Tazama vifaa na vichapishi katika Maunzi na Sauti.
    • Windows Vista
      Bofya kitufe cha kuwasha, na uteue Paneli Dhibiti > Kichapishi katika Maunzi na Sauti.
  2. Bofya kulia kwenye kichapishi chako na uteue Sifa.

  3. Teua kichupo cha Huduma ya Wavuti na ubofye URL.

    Kwa vile kichapishi kinatumia cheti cha kutiwa sahihi binafsi kufikia HTTPS, onyo huonyeshwa kwenye kivinjari unapoanza Web Config; hii haionyeshi kuwa kuna tatizo na unaweza kupuuza kwa usalama.