/ Kutayarisha Kichapishi / Kupakia Karatasi / Kupakia Bahasha na Tahadhari

Kupakia Bahasha na Tahadhari

Pakia bahasha ukingo mfupi kwanza katikati wakati upande wa kuchapisha unaangalia chini, na kisha telezesha miongozo ya ukingo wa mbele katika ukingo wa bahasha.

  • Pepeza na upange kingo za bahasha kabla ya kuzipakia.Wakati bahasha zilizokusanywa zimefurishwa na hewa, zifinye chini ili uzifanye tambarare kabla ya kuzipakia.

  • Usitumie bahasha ambazo zimekunjika au kukunjwa.Utumiaji wa bahasha hizi husababisha ukwamaji wa karatasi na uchafu kwenye uchapishaji.

  • Usitumie bahasha zilizo na sura zenye kunata kwenye kifuniko au dirisha la bahasha.

  • Epuka kutumia bahasha ambazo ni nyembamba sana, kwani zinaweza kukunjika wakati wa uchapishaji.