/ Kutayarisha Kichapishi / Kupakia Karatasi / Karatasi Inayopatikana na Uwezo / Tahadhari za Kushughulikia Karatasi

Tahadhari za Kushughulikia Karatasi

  • Soma karatasi ya maelekezo iliyokuja na karatasi.

  • Ili kufanikisha machapisho ya ubora wa juu kwa karatasi halali la Epson, tumia karatasi katika mazingira yaliyotajwa kwenye laha zilizotolewa kwa karatasi.

  • Pepeza na upange kingo za karatasi kabla ya kuzipakia. Usipepeze au kukunja karatasi ya picha. Kufanya hivyo kunaweza kuharibu upande wa kuchapisha.

  • Ikiwa karatasi imekunjwa, inyoroshe au ikunje kidogo upande huo mwingine kabla ya kupakia. Kuchapisha kwenye karatasi zilizokunjwa kunaweza kusababisha karatasi kukwamba na uchafu kwenye uchapishaji.

  • Usitumie karatassi ambayo ina mawimbi, imeraruka, imekatwa, kukunjwa, pwetepwete, nyembamba sana, au karatasi iliyo na mabango juu yake. Utumiaji wa aina hizi za karatasi husababisha ukwamaji wa karatasi na uchafu kwenye uchapishaji.

  • Hakikisha unatumia karatasi yenye punje refu. Ikiwa huna uhakika ni aina gani ya karatasi unayotumia, angalia ufungaji wa karatasi au wasiliana na mtengenezaji ili uthibitishe ainisho za karatasi.