/ Kuchapisha / Kuchapisha Kutoka kwa Vifaa Mahiri / Kuchapisha Ukitumia Mopria Print Service

Kuchapisha Ukitumia Mopria Print Service

Mopria Print Service huwezesha uchapishaji wa papo hapo wa pasi waya kutoka kwenye simu maizi au kompyuta ndogo za Android.

  1. Sakinisha Mopria Print Service kutoka Google Play.

  2. Pakia karatasi katika kichapishi.

  3. Sanidi kichapishi chako kwa uchapishi wa pasi waya. Tazama kiungo cha hapa chini.

    http://epson.sn

  4. Unganisha kifa chako cha Android kwenye mtandao sawa wa pasi waya ambao kichapishi chako kinatumia.

  5. Chapisha kutoka kwa kifaa chako hadi kwa printa.

    Kumbuka:

    Kwa maelezo zaidi, fikia tovuti ya Mopria Web katika https://mopria.org.