/ Mipangilio ya Mtandao / Kuunganisha kwenye Kompyuta

Kuunganisha kwenye Kompyuta

Tunapendekeza kutumia kisakinishaji ili kuunganisha kichapishi kwenye kompyuta. Unaweza kuendesha kisakinishaji kwa kutumia mbinu zifuatazo.

  • Kusanidi kutoka kwenye tovuti

    Fikia tovuti ifuatayo, kisha uingize jina la bidhaa. Nenda kwenye Mpangilio, na kisha uanze kusanidi.

    http://epson.sn

  • Sanidi kwa kutumia diski ya programu (kwenye modeli zinazokuja na diski ya programu na watumiaji walio na kompyuta za Windows zilizo na viendeshi vya diski pekee).

    Chomeka diski ya programu kwenye kompyuta, kisha ufuate maagizo ya kwenye skrini.

Uteuaji wa Mbinu za Muunganisho

Fuata maagizo ya kwenye skrini hadi skrini ifuatayo ionekane, na kisha teua njia ya muunganisho ya kichapishi kwenye kompyuta.

Teua aina ya muunganisho na kisha ubofye Ifuatayo.

Fuata maagizo ya kwenye skrini.