/ Kutuma Faksi / Kutuma Faksi Kutoka kwa Kompyuta / Kutuma Nyaraka Zilizoundwa kwa Kutumia Programu-tumizi (Mac OS)

Kutuma Nyaraka Zilizoundwa kwa Kutumia Programu-tumizi (Mac OS)

Kwa kuteua kichapishi kinachotuma faksi kutoka kwenye menyu ya Chapisho ya prohgramu-tumizi za kibiashara zinazopatikana, unaweza kutuma data kama vile nyaraka, michoro, na kompyuta ndogo, ulizounda.

Kumbuka:

Ufafanuzi unaofuata hutumia Uhariri wa Matini, programu-tumizi wastani ya Mac OS akama mfano.

  1. Unda waraka unaotaka kutuma kwa faksi kwenye programu-tumizi.

  2. Bofya Kuchapisha kutoka kwenye menyu ya Faili.

    Dirisha la programu-tumizi la Chapisho linaonyeshwa.

  3. Teua kichapishi chako (jina la faksi) kwenye Jina bofya ili kuonyesha mipangilio ya kina, angalia mipangilio ya chapisho, na kisha ubofye Sawa.

  4. Unda mipangilio kwa kila kipengee.

    • Bainisha 1 kwenye Idadi ya nakala. Hata iwapo utabainisha 2 au zaidi, nakala 1 tu inatumwa.
    • Unaweza kutuma hadi kurasa 100 katika usambazaji mmoja wa faksi.
    Kumbuka:

    Ukubwa wa ukurasa wa nyaraka unaoweza kutuma ni sawa na ukubwa wa karatasi unaoweza kutuma faksi kutoka kwenye kichapishi.

  5. Teua Fax Settings kutoka kwenye menyu ibukizi, na kisha uunde mipangilio kwa kila kipengee.

    Tazama msaada wa kiendeshi cha PC-FAX kwa ufafanuzi kwenye kila kipengee cha mpangilio.

    Bofya upande wa chini kushoto wa dirisha ili kufungua msaada wa kiendeshi cha PC-FAX.

  6. Teua menyu ya Recipient Settings, na kisha ubainishe mpokeaji.

    • Kubanisha mpokeaji (jina, faksi, nambari, nakadhalika) moja kwa moja:
      Bofya kipengee cha Add, ingiza maelezo yanayofaa, na kisha ubofye . Mpokeaji anaongezwa kwenye Recipient List iliyoonyeshwa sehemu ya juu ya dirisha.
      Iwapo umeteua “Enter fax number twice” kwenye mipangilio ya kiendeshi cha PC-FAX, unahitaji kuingiza nambari hiyo tena unapobofya .
      Iwapo laini ya muunganisho wa faksi yako inahitaji msimbo wa kiambishi awali, ingiza External Access Prefix.
      Kumbuka:

      Iwapo Aina ya Laini ya kichapishi chako imewekwa kwa PBX na msimbo wa ufikiaj umewekwa kwa # (hashi) badala ya kuingiza msimbo halisi wa kiambishi awali, ingiza # (hashi). Kwa maelezo, angalia Aina ya Laini kwenye Mipangilio Msingi kutoka kwenye kiungo cha maelezo Husiani hapa chini.

    • Kuteua mpokeaji (jina, faksi, nambari, nakadhalika) kutoka kwenye kitabu cha simu:
      Iwapo mpokeaji amehifadhiwa kwenye kitabu cha anwani, bofya . Teua mpokeaji kutoka kwenye orodha, na kisha ubofye Add > OK.
      Iwapo laini ya muunganisho wa faksi yako inahitaji msimbo wa kiambishi awali, ingiza External Access Prefix.
      Kumbuka:

      Iwapo Aina ya Laini ya kichapishi chako imewekwa kwa PBX na msimbo wa ufikiaj umewekwa kwa # (hashi) badala ya kuingiza msimbo halisi wa kiambishi awali, ingiza # (hashi). Kwa maelezo, angalia Aina ya Laini kwenye Mipangilio Msingi kutoka kwenye kiungo cha maelezo Husiani hapa chini.

  7. Angalia mipangilio ya mpokeaji, na kisha ubofye Fax.

    Inaanza kutuma.

    Hakikisha jina pamoja na nambari ya faksi ya mpokeaji ni sahihi kabla ya usambazaji.

    Kumbuka:
    • Iwapo utabofya ikoni ya kichapishi kwenye Dock, skrini ya kukagua hali ya usambazaji inaonyeshwa. Ili kusitisha kutuma, bofya data, na kisha ubofye Delete.

    • Iwapo kosa litatokea wakati wa usambazaji, ujumbe wa Sending failed unaonyeshwa. Angalia rekodi za usambazaji kwenye skrini ya Fax Transmission Record.

    • Huenda nyaraka zilizo na ukubwa uliochanganywa wa karatasi zisitumwe sahihi.