/ Kukarabati Kichapishi / Kuzuia Kukauka kwa Kichwa cha Kuchapisha

Kuzuia Kukauka kwa Kichwa cha Kuchapisha

Kila mara tumia kitufe cha nishati unapowasha na kuzima kichapishi.

Hakikisha kuwa taa ya nishati imezimwa kabla utenganisahe kamba ya nishati.

Wino wenyewe unaweza kukauka iwapo haujafunikwa. Kama tu kuweka kifuniko kwenye kalamu ya wino au kalamu ya mafuta ili kuizuia kukauka, hakikisha kichwa cha kuchapisha kimefunikwa vilivyo ili kuzuia wino kukauka.

Wakati kamba ya nishati imechomolewa au tatizo la nishati litokee wakati kichapishi kinaendeshwa, kichwa cha kuchapisha huenda kisifunikwe vilivyo. Iwapo kichwa cha kuchapisha kinasalia vivyo hivyo, kitakauka huku kikisababisha kuzibika kwa nozeli (sehemu za kutoa wino).

Katika hali hizi, washa na uzime kichapishi tena haraka iwezekanavyo ili kufunika kichwa cha kuchapisha.