/ Kutuma Faksi / Kupokea Faksi kwenye Kichapishi / Kupokea Faksi na Kupiga Simu / Kupokea Faksi kwa Uchaguzi (Itisha Hati)

Kupokea Faksi kwa Uchaguzi (Itisha Hati)

Unaweza kupokea faksi iliyohifadhiwa kwenye mashine nyingine ya faksi kwa kudayo nambari ya faksi. Tumia kipengele hiki kupokea hati kutoka kwa huduma ya maelezo ya faksi.

Kumbuka:
  • Iwapo huduma ya maelezo ya faksi ina kipengele cha mwongozo wa sikizi unachohitaji kufuata ili upokee waraka, huwezi kukitumia kipengele hiki.

  • Ili upokee hati kutoka kwa huduma ya maelezo ya faksi inayotumia mwongozo wa sikizi, dayo nambari ya faksi ukitumia simu iliyounganishwa, na utumie simu na printa ukifuata mwongozo wa sikizi.

  1. Teua Faksi kwenye skrini ya nyumbani.

    Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya , na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  2. Bonyeza kitufe cha Sawa, na kisha uteue Zaidi.

  3. Teua Itisha Hati, na kisha uteue Washa.

  4. Bainisha mpokeaji.

    Kumbuka:

    Iwapo huwezi kuingiza nambari ya faksi kikuli, Vikwazo vya Kupiga Moja kwa moja kwenye Mipangilio ya Usalama imewekwa kwa Washa. Teua wapokeaji wa faksi kutoka kwenye orodha ya waasiliani au historia ya faksi iliyotumwa.

  5. Bonyeza kitufe cha ili uanze Itisha Hati.