Kufikia Kiendeshi cha Kichapishi

Unapofikia kiendeshi cha kichapishi kutoka kwenye paneli dhibiti ya kompyuta, mipangilio inatekelezwa kwa programu-tumizi zote.

Kufikia kiendeshi cha printa kutoka kwa paneli dhibiti
  • Windows 10/Windows Server 2019/Windows Server 2016

    Bofya kitufe cha kuwasha, na uteue Mfumo wa Windows > Paneli Dhibiti > Tazama vifaa na vichapishi kwenye Maunzi na Sauti. Bofya kulia kwenye kichapihsi chako, au bonyeza na uishikilie na kisha uchague Mapendeleo ya uchapishaji.

  • Windows 8.1/Windows 8/Windows Server 2012 R2/Windows Server 2012

    Teua Eneo Kazi > Mipangilio > Paneli Dhibiti > Tazama vifaa na vichapishi katika Maunzi na Sauti. Bofya kulia kwenye kichapihsi chako, au bonyeza na uishikilie na kisha uchague Mapendeleo ya uchapishaji.

  • Windows 7/Windows Server 2008 R2

    Bofya kitufe cha kuwasha, na uteue Paneli Dhibiti > Tazama vifaa na vichapishi katika Maunzi na Sauti. Bofya kulia kwenye kichapishi chako na uteue Mapendeleo ya kichapishi.

  • Windows Vista/Windows Server 2008

    Bofya kitufe cha kuwasha, na uteue Paneli Dhibiti > Kichapishi katika Maunzi na Sauti. Bofya kulia kwenye kichapishi chako na uteue Mapendeleo ya kichapishi.

  • Windows XP/Windows Server 2003 R2/Windows Server 2003

    Bofya kitufe cha kuwasha, na uteue Paneli Dhibiti > Vichapishi na Maunzi Nyingine > Vichapishi na Faksi. Bofya kulia kwenye kichapishi chako na uteue Mapendeleo ya kichapishi.

Kufikia kiendeshi cha printa kutoka kwa ikoni ya printa kwenye mwambaa kazi

Ikoni ya printa iliyo kwenye mwambaa kazi wa eneo kazi ni ikoni ya mkato ya kukuwezesha ufikie kiendeshi cha printa kwa urahisi.

Ukibofya ikoni ya printa na uchague Mipangilio ya Printa, unaweza kufikia dirisha sawa la mipangilio ya printa na linaloonekana katika paneli dhibiti. Ukibofya ikoni hii mara mbili, unaweza kuona hali ya printa.

Kumbuka:

Ikiwa ikoni ya printa haionekani kwenye mwabaa kazi, nenda kwa dirisha la kiendeshi cha printa, bofya Inachunguza Mapendeleo kwenye kichupo cha Utunzaji, na kisha uchague Sajili ikoni ya njiamkato kwenye upau kazi.