/ Kubadilisha Vibweta vya Wino na Bidhaa Zingine za MMatumizi / Kuhifadhi Wino Mweusi wakati Wino Mweusi Umepungua (kwa Windows Pekee)

Kuhifadhi Wino Mweusi wakati Wino Mweusi Umepungua (kwa Windows Pekee)

Wakati wino mweusi unapungua na kuna wino wa rangi wa kutosha unaobakia, unaweza kutumia mchanganyiko wa wino wa rangi ili kuunda wino mweusi. Unaweza kuendelea kuchapisha unapoandaa kubadilisha kibweta cha wino mweusi.

Kipengele hiki kinapatikana tu wakati unateua mipangilio ifuatayo kwenye kiendeshi cha kichapishi.

  • Aina ya Krtasi: Karatasi tupu

  • Ubora: Wastani

  • EPSON Status Monitor 3: Imewezeshwa

Kumbuka:
  • Ikiwa EPSON Status Monitor 3 imelemazwa, nenda kwa kiendeshi cha printa, bofya Mipangilio Iliyorefushwa katika kichupo cha Utunzaji, na kisha uchague Wezesha EPSON Status Monitor 3.

  • Mchanganyiko wa mitazamo nyeusi inatofautiana kiasi na weusi kamili. Zaidi ya hayo, kasi ya kuchapisha inapungua.

  • Ili kudumisha ubora wa kichwa cha kuchapisha, kadhalika, wino mweusi unatumika.

Chaguo

Ufafanuzi

Ndiyo

Teua ili utumie mchanganyiko wa wino wa rangi ili kuunda rangi nyeusi. Dirisha hili linaonyeshwa wakati mwingine unachapisha kazi kama hiyo.

La

Teua ili kuendelea kutumia wino mweusi unaosalia. Dirisha hili linaonyeshwa wakati mwingine unachapisha kazi kama hiyo.

Lemaza kipengele hiki

Teua ili kuendelea kutumia wino mweusi unaosalia. Dirisha hili halionyeshwi hadi ubadilishe kibweta cha wino mweusi na upungue tena.