/ Kutayarisha Kichapishi / Kudhibiti Waasiliani / Kisajili au Kuhariri Waasiliani wa Kikundi

Kisajili au Kuhariri Waasiliani wa Kikundi

Kuongeza anwani kwa kundi kunakuwezesha kutumia faksi kwa miishilio mbalimbali kwa wakati mmoja.

  1. Teua Mipangilio kwenye skrini ya nyumbani.

    Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya , na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  2. Teua Kisimamia Waasiliani.

  3. Fanya moja kati ya zifuatazo.

    • Ili kusajili kikundi kipya cha waasiliani, teua Ongeza Kikundi, na kisha uteue nambari ya usajili.
    • Ili kuhariri kikundi cha waasiliani, teua Hariri, na kisha uteue kikundi lengwa.
    • Ili kufuta waasiliani wa kikundi, teua Futa, teua kikundi kinacholengwa, na kisha uteue Ndiyo. Hakuna hatua za ziada zinazohitajika.
  4. Ingiza au hariri Jina la Kikundi, na kisha uteue OK.

  5. Ingiza au hariri Neno la Kiolesura, na kisha uteue OK.

  6. Teua waasiliani unaotaka kusajili katika kundi.

    Kila wakati unaponyeza kitufe cha , mwasiliani anateuliwa na kuondolewa uteuzi kwa wakati mmoja.

    Kumbuka:

    Unaweza kuzajili hadi waasiliani 99.

  7. Teua Ongeza Ingizo ili kukamilisha kujisajili au kuhariri.