/ Mipangilio ya Faksi / Kuunganisha Printa Kwenye Laini ya Simu / Kuunganisha Printa Kwenye Laini ya Simu

Kuunganisha Printa Kwenye Laini ya Simu

Unganisha printa kwenye soketi ya simu ya ukutani kwa kutumia kebo ya simu ya RJ-11 (6P2C). Wakati unaunganisha simu kwenye printa, tumia kebo ya simu ya RJ-11 (6P2C).

Kulingana na eneo lako, huenda kebo ya simu ikajumuisha na printa. Ikiwa imejumuishwa, tumia kebo hiyo.

Huenda ukahitajika kuunganisha kebo ya simu kwenye adapta iliyotolewa kwa nchi au eneo lako.

Kumbuka:

Ondoa kituniko kutoka kwa lango la EXT. la printa peke yake unapounganisha simu yako kwenye printa. Usiondoe kifuniko ikiwa huunganishi simu yako.

Katika maeneo ambayo huwa na radi mara kwa mara, tunapendekeza kwamba utumie kizuia mfuro wa umeme.