/ Huduma ya Mtandao na Maelezo ya Programu / Programu ya Uchapishaji Haraka na Furaha kutoka katika Kompyuta (Epson Photo+)

Programu ya Uchapishaji Haraka na Furaha kutoka katika Kompyuta (Epson Photo+)

Epson Photo+ ni programu inayokuruhusu kuchapisha picha kwa urahisi kwa miundo tofauti. Unaweza kutumia violezo anuwai na kufanya marekebisho ya taswira na kurekebisha mkao unapotazama uhakiki wa waraka wako. Pia unaweza kuongeza mwangaza kwenye taswira zako kwa kuongeza matini na mihuri unapopenda. Unapochapisha kwenye karatasi hjalali la picha la Epson, utendaji wa wino unetumika kwa upeo wa juu kuunda ukamilisho maridadi kwa rangi nzuri zaidi.

Pia inakuja na vipengele vifuatavyo. Angalia msaada wa programu kwa maelezo. Unaweza kupakua programu-tumizi za sasa kutoka kwenye tovuti ya Epson.

http://www.epson.com

  • Lebo za diski ya kuchapisha (mifumo inayoauniwa pekee)

  • Misimbo ya QR iliyoundwa ya kuchapisha

  • Kuchapisha picha zinazoonyesha tarehe na saa ya kupiga

Kumbuka:
  • Programu endeshi za Windows Server hazikubaliwi.

  • Ili utumie programu hii kiendeshji cha kichapishi kinahitaji kusakinishwa.

Kuanzia kwenye Windows
  • Windows 10

    Bofya kitufe cha kuwasha kisha uteue Epson Software > Epson Photo+.

  • Windows 8.1/Windows 8

    Andika jina la programu katika sehemu ya utafutaji, na kisha uchague ikoni inayoonekana.

  • Windows 7

    Bofya kitufe cha kuwasha kisha uteue Programu Zote au Programu > Epson Software > Epson Photo+.

Kuanzia kwenye Mac OS

Teua Nenda > Programu > Epson Software > Epson Photo+.