/ Huduma ya Mtandao na Maelezo ya Programu / Programu ya Kusasisha Programu na Vifaa Dhibiti (Epson Software Updater)

Programu ya Kusasisha Programu na Vifaa Dhibiti (Epson Software Updater)

Epson Software Updater ni programu ambayo husakinisha programu mpya na kusasisha vifaa dhabiti na miongozo kupitia Mtandao. Iwapo unataka kuangalia taarifa ya visasisho mara kwa mara, unaweza kuweka kipindi cha kuangalia visasisho kwenye Mipangilio ya Epson Software Updater ya Sasisho Otomatiki.

Kumbuka:

Programu endeshi za Windows Server hazikubaliwi.

Kuanzia kwenye Windows
  • Windows 10

    Bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue EPSON Software > Epson Software Updater.

  • Windows 8.1/Windows 8

    Andika jina la programu katika sehemu ya utafutaji, na kisha uchague ikoni inayoonekana.

  • Windows 7/Windows Vista/Windows XP

    Bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue Programu Zote (au Programu) > EPSON Software > Epson Software Updater.

Kumbuka:

Kadhalika, unaweza kuwasha Epson Software Updater kwa kubofya ikoni ya kichapishi kwenye mwambaa kazi ulio kwenye eneo kazi, na kisha uteue Kisasisho cha Programu.

Kuanzia kwenye Mac OS

Teua Nenda > Programu > Epson Software > Epson Software Updater.