/ Mipangilio ya Mtandao / Kukata muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi) Muunganisho kutoka kwenye Paneli Dhibiti

Kukata muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi) Muunganisho kutoka kwenye Paneli Dhibiti

Kuna mbinu mbili zinazopatikana za kulemaza muuganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi); unaweza kulemaza miunganisho yote kwa kutumia paneli dhibiti ya kichapishi, au kulemaza kila muunganisho kutoka kwenye kompyuta au kifaa maizi. Sehemu hii hufafanua jinsi ya kulemaza miunganisho yote.

Muhimu:

Wakati muunganisho wa Wi-Fi Direct wa (AP Rahisi) unalemazwa, kompyuta zote na vifaa maizi vilivyounganishwa kwenye kichapishi katika muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi) vinatenganishwa.

Kumbuka:

Iwapo unataka kukata muunganisho wa kifaa maalum, kata muunganisho kutoka kwenye kifaa badala ya kichapishi. Tumia mojawapo ya mbinu zifuatazo ili kukata muunganisho wa Wi-Fi Direct (AP Rahisi) kutoka kwenye kifaa.

  • Kata muunganisho wa Wi-Fi kwenye jina la mtandao la kichapishi (SSID).

  • Unganisha kwenye jina jingine la mtandao (SSID).

  1. Teua Usanidi wa Wi-Fi kwenye skrini ya nyumbani.

    Ili kuteua kipengee, tumia vitufe vya , na kisha ubonyeze kitufe cha OK.

  2. Teua Wi-Fi Direct.

  3. Bonyeza kitufe cha Sawa ili kuendelea.

  4. Bonyeza kitufe cha Sawa ili kuendelea.

  5. Bonyeza kitufe cha ili kuonyesha skrini ya mpangilio.

  6. Teua Lemaza Wi-Fi Direct.

  7. Thibitisha ujumbe, na kisha ubonyeze kitufe cha Sawa.