/ Kutatua Matatizo / Matatizo ya Uchapishaji / Ubora wa Uchapishaji Uko Chini

Ubora wa Uchapishaji Uko Chini

Angalia yafuatayo ikiwa ubora wa uchapishaji uko chini kwa sababu ya uchapishaji wenye ukungu, mistari, rangi zinakosekana, kutolingana, katika uchapishaji.

Kukagua kichapishi
  • Fanya ukaguzi wa nozeli, na kisha usafishe kichwa cha kuchapisha ikiwa nozeli zozote za kichwa cha kichapisha zitaziba.

  • Linganisha kichwa cha kuchapisha.

Kukagua karatasi
  • Tumia karatasi inayokubailiwa na hiki kichapishi.

  • Usichapishe kwenye karatasi pwetepwere, iliyoharibika, au iliyozeeka sana.

  • Ikiwa karatasi imekunjika au bahasha imejaa hewa, ilanyoroshe.

  • Usiwekele karatasi juu ya zingine mara tu baada ya kuchapisha.

  • Kausha uchapishaji kabisa kabla ya kuziweka kwenye rekodi au kuzionyesha. Wakati unakausha uchapishaji, usiziweke kwenye mwale wa jua wa moja kwa moja, na usitumie mashine ya kukaushia, na usiguse upande wa karatasi uliochapishwa.

  • Wakati unachapisha picha, Epson inapendekeza utumie karatasi halali ya Epson mbali na karatasi tupu. Chapisha upande unaoweza kuchapishwa wa karatasi halali ya Epson.

Kukagua mipangilio ya kichapishi
  • Teua mpangilio unaofaa wa aina ya karatasi kwa aina ya karatasi iliyopakiwa katika kichapishi.

  • Chapisha kwa kutumia mpangilio wa ubora wa juu.

Kukagua kibweta cha wino
  • Epson inapendekeza utumie katriji ya wino kabla ya tarehe iliyochapishwa kwenye pakiti.

  • Kwa matokeo mazuri zaidi, tumia wino wote katika katriji ya wino ndani ya miezi sita baada ya kufungua pakiti.

  • Jaribu kutumia katriji halali za wino za Epson. Bidhaa hii imeundwa kurekebisha rangi kulingana na matumizi ya katriji halali za wino za Epson. Kutumia katriji zisizo halali za wino kunaweza kusabbaisha kupungua kwa ubora wa uchapishaji.