/ Huduma ya Mtandao na Maelezo ya Programu / Programu-tumizi ya Kusanidi Operesheni za Utambazaji kutoka kwa Paneli Dhibiti (Epson Event Manager)

Programu-tumizi ya Kusanidi Operesheni za Utambazaji kutoka kwa Paneli Dhibiti (Epson Event Manager)

Epson Event Manager ni programu-tumizi inayokuruhusu kudhibiti utambazaji kutoka kwa paneli dhibiti na kuhifadhi picha kwenye kompyuta.Unaweza kuongeza mipangilio yako mwenyewe kama mipangilio ya kabla, kama vile aina ya waraka, eneo la kabrasha la hifadhi, na umbizo la taswira.Angalia msaada wa programu-tumizi kwa maelezo.

Kumbuka:

Mifumo Windows Server ya kuendesha haiauniwi.

Kuanzia kwenye Windows
  • Windows 10

    Bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue Epson Software > Event Manager.

  • Windows 8.1/Windows 8

    Andika jina la programu-tumizi katika sehemu ya utafutaji, na kisha uteue ikoni inayoonekana.

  • Windows 7/Windows Vista/Windows XP

    Bofya kitufe cha kuwasha, na kisha uteue Programu Zote au Programu > Epson Software > Event Manager.

Kuanzia kwenye Mac OS

Nenda kwenye > Programu-tumizi > Epson Software > Event Manager.