Kuendesha Web Config kwenye Mac OS

  1. Teua Mapendeleo ya Mfumo kwenye menyu ya Apple > Vichapishaji na Vitambazaji (au Chapisha na Utambaze, Chapisha na Utume Faksi), kisha uteue kichapishaji.

  2. Bofya Chaguo na Usambazaji > Onyesha Tovuti ya Kichapishi.

    Kwa vile kichapishi kinatumia cheti cha kutiwa sahihi binafsi kufikia HTTPS, onyo huonyeshwa kwenye kivinjari unapoanza Web Config; hii haionyeshi kuwa kuna tatizo na unaweza kupuuza kwa usalama.